Search This Blog

Saturday, March 18, 2017

Lishe ya ubongo

Kuna muda wa kufikiria kupanda mti fulani. Kuna mda wa kuamini kuwa unaweza kupanda mti huo na ukapata mazao. Kuna muda wa kwenda dukani kununua mbegu na pembejeo nyengine. Kuna muda wa kuatika mbegu ukasubiria iwe mche. Kuna muda wa kulima, kuweka matuta na kutoa magugu. Kuna muda wa kuweka mbolea. Kuna muda wa kuhamisha mche kupeleka shambani. Kuna muda wa kumwagilia. Kuna muda wa kutilia dawa mti ili wadudu wabaya wasidhuru. Kuna muda wa kupalilia. Kuna muda wa mti kutoa tunda na kuna muda wa kusubiria ili uvune. Kuna muda wa kutoa zao shambani mpaka sokoni. Kuna muda wa kuuza mazao yako. Kuna muda wa kuchanganua mahesabu na kuweka mtaji mbali na faida mbali. Kuna muda wa kutumia faida yako. Hizo zote ni process zinazochukua mda, na huwezi kufanya pupa ili kufikia mwisho vingevyo utaharibu. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye ndoto zetu au zaidi inatupasa tuwe na subra, hekima na busara ili tuweze kufika kule tunapotaka kufika.
By juma salim